sw_tn/lev/09/22.md

633 B

kisha akashuka chini

Kirai "akashuka chini" kimetumika kwa sababu mahali pa madhabahu palikuwa juu zaidi ya mahali watu walipokuwa wanasimama.

utukufu wa Yahweh ukaonekana kwa watu wote

"Utukufu" hapa huwakilisha uwepo wa Yahweh. : "Yahweh akawaonyesha watu wote utukufu wa uwepo wake"

Moto ukashuka kutoka kwa Yahweh na ukairamba

"Yahweh alituma moto ulioiramba"

ukairamba sadaka ya kuteketezwa

Moto ukiitekeza kabisa sadaka umezungumziwa kana kwamba moto uiitafuna au kuitumia sadaka ya kutekezwa.

wakala wakiinamisha nyuso zao chini

"walilala wakaelekeza nyuso zao ardhini." Hii ni ishara ya heshima na adhama.