# kisha akashuka chini Kirai "akashuka chini" kimetumika kwa sababu mahali pa madhabahu palikuwa juu zaidi ya mahali watu walipokuwa wanasimama. # utukufu wa Yahweh ukaonekana kwa watu wote "Utukufu" hapa huwakilisha uwepo wa Yahweh. : "Yahweh akawaonyesha watu wote utukufu wa uwepo wake" # Moto ukashuka kutoka kwa Yahweh na ukairamba "Yahweh alituma moto ulioiramba" # ukairamba sadaka ya kuteketezwa Moto ukiitekeza kabisa sadaka umezungumziwa kana kwamba moto uiitafuna au kuitumia sadaka ya kutekezwa. # wakala wakiinamisha nyuso zao chini "walilala wakaelekeza nyuso zao ardhini." Hii ni ishara ya heshima na adhama.