sw_tn/lev/02/04.md

28 lines
969 B
Markdown

# Taarifa kwa ujumla
Yahweh anaendelea kumwambia Musa kwamba watu hao pamoja na makuhani yawapasa wafanye hivyo ili sadaka zao ziweze kukubalika kwake.
# uliookwa kweye tanuru
Sentensi hii yaweza kutamkwa katika mtindo tendaji. : "uliouoka kwenye tanuru"
# tanuru
Huenda hiki kilikuwa ni chombo kilichotengenezwa kwa udongo chenye uwazi shimo katikati. Moto uliwashwa chini ya tanuru, na joto lingeoka donge la unga ndani ya tanuru.
# mkate laini wa unga safi
yaeleweka kwamba mkate laini haukuwa na hamira.
# uliopakwa mafuta
Tafsiri kirai hiki kuonesha kwamba mafuta ni lazima yapakwe kwenye mkate. :"pamoja na mafuta juu ya mkate"
# Iwapo toleo lako la nafaka limeokwa kwa kikaango cha chuma
Hii yaweza kutamkwa katika mtindo tendaji. : Iwapo unaioka sadaka yako ya nafaka katika kiaango cha chuma"
# kikaango cha chuma
Hii ni sahani nzito iliyotengenezwa ama kwa udongo au chuma. Sahani iliwekwa juu ya moto, na donge la ungu lilipikwa juu ya sahani.