# Taarifa kwa ujumla Yahweh anaendelea kumwambia Musa kwamba watu hao pamoja na makuhani yawapasa wafanye hivyo ili sadaka zao ziweze kukubalika kwake. # uliookwa kweye tanuru Sentensi hii yaweza kutamkwa katika mtindo tendaji. : "uliouoka kwenye tanuru" # tanuru Huenda hiki kilikuwa ni chombo kilichotengenezwa kwa udongo chenye uwazi shimo katikati. Moto uliwashwa chini ya tanuru, na joto lingeoka donge la unga ndani ya tanuru. # mkate laini wa unga safi yaeleweka kwamba mkate laini haukuwa na hamira. # uliopakwa mafuta Tafsiri kirai hiki kuonesha kwamba mafuta ni lazima yapakwe kwenye mkate. :"pamoja na mafuta juu ya mkate" # Iwapo toleo lako la nafaka limeokwa kwa kikaango cha chuma Hii yaweza kutamkwa katika mtindo tendaji. : Iwapo unaioka sadaka yako ya nafaka katika kiaango cha chuma" # kikaango cha chuma Hii ni sahani nzito iliyotengenezwa ama kwa udongo au chuma. Sahani iliwekwa juu ya moto, na donge la ungu lilipikwa juu ya sahani.