sw_tn/lev/02/04.md

969 B

Taarifa kwa ujumla

Yahweh anaendelea kumwambia Musa kwamba watu hao pamoja na makuhani yawapasa wafanye hivyo ili sadaka zao ziweze kukubalika kwake.

uliookwa kweye tanuru

Sentensi hii yaweza kutamkwa katika mtindo tendaji. : "uliouoka kwenye tanuru"

tanuru

Huenda hiki kilikuwa ni chombo kilichotengenezwa kwa udongo chenye uwazi shimo katikati. Moto uliwashwa chini ya tanuru, na joto lingeoka donge la unga ndani ya tanuru.

mkate laini wa unga safi

yaeleweka kwamba mkate laini haukuwa na hamira.

uliopakwa mafuta

Tafsiri kirai hiki kuonesha kwamba mafuta ni lazima yapakwe kwenye mkate. :"pamoja na mafuta juu ya mkate"

Iwapo toleo lako la nafaka limeokwa kwa kikaango cha chuma

Hii yaweza kutamkwa katika mtindo tendaji. : Iwapo unaioka sadaka yako ya nafaka katika kiaango cha chuma"

kikaango cha chuma

Hii ni sahani nzito iliyotengenezwa ama kwa udongo au chuma. Sahani iliwekwa juu ya moto, na donge la ungu lilipikwa juu ya sahani.