sw_tn/job/01/06.md

37 lines
1.2 KiB
Markdown

# siku ambayo
Hii haikuwa siku maalumu. Kusanyiko lilifanyika mara kwa mara. "wakati ambapo" au "siku moja wakati"
# watoto wa Mungu
Hii inamaanisha malaika, viumbe wa mbinguni.
# kujihudhurisha mbele za BWANA
"kusimama pamoja mbele za BWANA kama alivyo waagiza kufanya"
# Natoka kuzunguka zunguka duniani, kutembea huku na huko humo
Msemo "kuzunguka zunguka" na "kutembea huku na huko" inakusudia kazi moja ya kusisitiza ukamilifu wake. "Kutoka mahali popote duniani."
# BWANA
Hili ni jina la Mungu ambalo alilifunua kwa watu wake katika Agano la Kale. Tazama ukurasa wa tafsiri ya Neno Yahweh kuhusu namna ya kulitafsiri
# kutembea huku na huko humo
"huku na huko" inahusian na kusafiri juu ya dunia yote.
# Je umemwangalia mtumishi wangu Ayubu?
"Je umefikiri kuhusu mtumishi wangu Ayubu?"
Hapa Mungu alianza kuzungumza na Shetani kuhusu Ayubu. "Angalia mtumishi wangu Ayubu"
# mtu mwenye haki na mkamilifu
Neno "mwenye haki" na "mkamilifu" yana maana sawa na yanaeleza kwamba Ayubu alikuwa muadilifu. "Alitenda yaliyo mema mbele za Mungu."
# mmoja aliyemcha Mungu na kuepukana na uovu
"mmoja aliyemheshimu Mungu" na "alikataa kufanya uovu." Hapa uovu unazungumziwa kama vile eneo ambalo mtu ataepuka kwenda huko, badala ya kufanya matendo maovu