# siku ambayo Hii haikuwa siku maalumu. Kusanyiko lilifanyika mara kwa mara. "wakati ambapo" au "siku moja wakati" # watoto wa Mungu Hii inamaanisha malaika, viumbe wa mbinguni. # kujihudhurisha mbele za BWANA "kusimama pamoja mbele za BWANA kama alivyo waagiza kufanya" # Natoka kuzunguka zunguka duniani, kutembea huku na huko humo Msemo "kuzunguka zunguka" na "kutembea huku na huko" inakusudia kazi moja ya kusisitiza ukamilifu wake. "Kutoka mahali popote duniani." # BWANA Hili ni jina la Mungu ambalo alilifunua kwa watu wake katika Agano la Kale. Tazama ukurasa wa tafsiri ya Neno Yahweh kuhusu namna ya kulitafsiri # kutembea huku na huko humo "huku na huko" inahusian na kusafiri juu ya dunia yote. # Je umemwangalia mtumishi wangu Ayubu? "Je umefikiri kuhusu mtumishi wangu Ayubu?" Hapa Mungu alianza kuzungumza na Shetani kuhusu Ayubu. "Angalia mtumishi wangu Ayubu" # mtu mwenye haki na mkamilifu Neno "mwenye haki" na "mkamilifu" yana maana sawa na yanaeleza kwamba Ayubu alikuwa muadilifu. "Alitenda yaliyo mema mbele za Mungu." # mmoja aliyemcha Mungu na kuepukana na uovu "mmoja aliyemheshimu Mungu" na "alikataa kufanya uovu." Hapa uovu unazungumziwa kama vile eneo ambalo mtu ataepuka kwenda huko, badala ya kufanya matendo maovu