sw_tn/jhn/18/intro.md

1.5 KiB

Yohana 18 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Mistari ya 13 na 14 inasema, "kwa kuwa alikuwa baba mkwe Kayafa, ambaye alikuwa kuhani mkuu mwaka huo. Sasa Kayafa ndiye aliyewapa Wayahudi ushauri kwamba ingekuwa bora kwamba mtu mmoja afe kwa ajili ya watu . " Hii ni taarifa ya mabano inayotolewa na mwandishi. Inalenga kuelezea taarifa muhimu ya historia. Inawezekana kuweka taarifa hii kwa mabano.

Dhana maalum katika sura hii

"Sio halali kwetu kumwua mtu yeyote"

Ufalme wa Kirumi haukuruhusu Wayahudi kutekeleza adhabu ya kifo kwa mtu yeyote. Kwa hiyo, Wayahudi walipaswa kuwasilisha kesi yao kwa mtawala wa kipagani, Pilato.

Ufalme wa Yesu

Yesu anamwelezea Pilato kwamba ufalme wake sio "wa ulimwengu huu." Wataalamu wengine huchukua hii kumaanisha ya kwamba Yesu anatawala ufalme wa kiroho, lakini wengine wanasema kama maana ya maneno ya Yesu ilikuwa kama ufalme wake haukushindana na ufalme wa Kirumi. Inawezekana kutafsiri maneno haya kama ufalme wa Yesu "haukuanzisha mahali hapa au huanzisha mahali pengine."

Mifano muhimu ya usemi katika sura hii

"Mfalme wa Wayahudi"

Maneno haya hutumiwa kwa njia mbili tofauti katika kifungu hiki. Kwanza, Yesu anasemekana kuwa mfalme wa Wayahudi. Yeye ndiye mfalme wa Wayahudi na ulimwengu wote. Pili, hutumiwa kwa kinaya au kudhihaki na Pilato. Pilato hakumwamini Yesu kuwa mfalme wa Wayahudi. (See: rc://*/ta/man/translate/figs-irony)

<< | >>