sw_tn/jhn/09/intro.md

1.9 KiB

Yohana 09 Maelezo ya Jumla

Dhana maalum katika sura hii

"Ni nani aliyetenda dhambi?"

Katika Israeli ya kale, mara nyingi waliamini kwamba mtoto alizaliwa na ulemavu kwa sababu ya dhambi ya mmoja wa wazazi wake. Hii haikuwa mafundisho ya sheria ya Musa. Katika mjadala huu, Mafarisayo walikuwa wenye dhambi kwa sababu waliona uwezo wa Yesu na hawakumuabudu. (See: [[rc:///tw/dict/bible/kt/sin]] and [[rc:///tw/dict/bible/kt/lawofmoses]]).

Mimi mdimi

Yohana anatumia maneno haya mara saba katika injili yake. Ni maneno sawa yanayotumiwa na Mungu, alipojidhihirisha pamoja na jina lake Yahweh katika kichaka kilichokuwa kinawaka. Jina "Yahweh" linaweza kutafsiriwa kama "Mimi ndimi."

Mwangaza

Mwangaza ni mfano wa kawaida katika Maandiko yaliyotumiwa kuonyesha haki. Mwangaza pia hutumiwa kuonyesha njia ya haki na kuonyesha maisha ya haki. Giza hutumiwa mara nyingi kama mfano unaonyesha dhambi au uovu. (See: [[rc:///tw/dict/bible/other/light]], [[rc:///tw/dict/bible/kt/righteous]], [[rc:///tw/dict/bible/other/darkness]], [[rc:///tw/dict/bible/kt/sin]] and rc://*/tw/dict/bible/kt/unrighteous)

"Yeye haishiki Sabato"

Mafarisayo walimwona Yesu akifanya matope kuwa "kazi" na kukiuka sheria kuhusu Sabato. (See: rc://*/tw/dict/bible/kt/sabbath)

Mifano muhimu ya usemi katika sura hii

Kuona

Katika sura hii kumeandikwa habari ya mtu aliyezaliwa kipofu. Yesu pia anatumia habari hizi kama mfano. Katika Yohana 9:39-40, Mafarisayo wanaitwa vipofu kwa sababu hawawezi kuona ukweli ulio mbele yao. (See: rc://*/ta/man/translate/figs-metaphor)

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

"Mwana wa Binadamu"

Yesu anajiita mwenyewe kama "Mwana wa Binadamu." Lugha zingine haziwezi kuruhusu mtu kujitaja mwenyewe kama 'mtu wa tatu.' (See: rc://*/tw/dict/bible/kt/sonofman)

<< | >>