sw_tn/jhn/08/intro.md

1.5 KiB

Yohana 08 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Watafsiri wanaweza kupenda kuandika alama katika mstari wa 1 ili kuelezea msomaji kwa nini wamechagua kutafsiri au kutotafsiri mistari 8:1-11. Kwa sababu hiki ni kifungu cha utata, ni bora kutokuwa na hitimisho la kitheolojia kutoka kwa kifungu hiki.

Dhana maalum katika sura hii

Mwangaza

Mwangaza ni mfano ya kawaida katika Maandiko yaliyotumiwa kuonyesha haki. Mwangaza pia hutumiwa kuonyesha njia ya haki na kuonyesha maisha ya haki. Giza hutumiwa mara nyingi kama mfano zinazowakilisha dhambi au uovu. (See: [[rc:///tw/dict/bible/other/light]], [[rc:///tw/dict/bible/kt/righteous]],

Mimi ndimi

Yohana anatumia maneno haya mara saba katika injili yake. Ni maneno sawa yanayotumiwa na Mungu, alipojidhihirisha pamoja na jina lake Yahweh katika kichaka kilichokuwa kinawaka. Jina "Yahweh" linaweza kutafsiriwa kama "Mimi ndimi."

"Mwanamke aliyekamatwa katika kitendo cha uzinzi"

Ikiwa mwanamke huyo alipatwa katika kitendo cha uzinzi, kulikuwa na mwanamume ambaye pia alikamatwa katika kitendo cha uzinzi. Mwanamume huyo hayuko katika maelezo haya. (See: [[rc:///tw/dict/bible/kt/adultery]] and [[rc:///ta/man/translate/figs-explicit]])

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

"Mwana wa Binadamu"

Yesu anajiita mwenyewe kama "Mwana wa Binadamu." Lugha zingine haziwezi kuruhusu mtu kujitaja mwenyewe kama 'mtu wa tatu.'

<< | >>