sw_tn/jdg/03/09.md

924 B

Bwana akamuinua mtu

Bwana akamchagua mtu kufanya kazi maalumu kwa ajili yake.

Othnieli ... Kenazi

Majina haya ni ya wanaume.

akamtia nguvu

Maneno haya yanamaanisha kwamba Bwana akamsaidia Othnieli kukuza sifa alizozitaka ili awe kiongozi bora.

akahukumu Israeli

"kuhukumu" inamaanisha kuwaongoza wana wa Israeli.

naye akatoka kwenda vitani

"naye" inamuelezea Othnieli ambaye anawakilisha jeshi la Israeli. "Othnieli na jeshi la Israeli wakatoka kwenda kupigana na jeshi la Kushan-rishathaimu"

Bwana akampa kuishinda Kush-rishataimu mfalme wa Aramu

"Kush-rishataimu" anawakilisha jeshi lake. "Bwana akalisaidia jeshi la Israeli kulishinda jeshi la Kush-rishataimu mfalme wa Aramu"

Mkono wa Othnieli

Hapa neno "mkono" limesimama badala ya jeshi. "Jeshi la Othnieli"

Nchi ilikuwa na amani

"nchi" imetumika kuelezea watu waishio ndani yake. "Watu waliishi kwa amani"

Miaka arobaini

"miaka 40"