sw_tn/jdg/03/09.md

36 lines
924 B
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2019-05-21 20:17:16 +00:00
# Bwana akamuinua mtu
Bwana akamchagua mtu kufanya kazi maalumu kwa ajili yake.
# Othnieli ... Kenazi
Majina haya ni ya wanaume.
# akamtia nguvu
Maneno haya yanamaanisha kwamba Bwana akamsaidia Othnieli kukuza sifa alizozitaka ili awe kiongozi bora.
# akahukumu Israeli
"kuhukumu" inamaanisha kuwaongoza wana wa Israeli.
# naye akatoka kwenda vitani
"naye" inamuelezea Othnieli ambaye anawakilisha jeshi la Israeli. "Othnieli na jeshi la Israeli wakatoka kwenda kupigana na jeshi la Kushan-rishathaimu"
# Bwana akampa kuishinda Kush-rishataimu mfalme wa Aramu
"Kush-rishataimu" anawakilisha jeshi lake. "Bwana akalisaidia jeshi la Israeli kulishinda jeshi la Kush-rishataimu mfalme wa Aramu"
# Mkono wa Othnieli
Hapa neno "mkono" limesimama badala ya jeshi. "Jeshi la Othnieli"
# Nchi ilikuwa na amani
"nchi" imetumika kuelezea watu waishio ndani yake. "Watu waliishi kwa amani"
# Miaka arobaini
"miaka 40"