sw_tn/jas/05/intro.md

1.2 KiB

Yakobo 05 Maelezo kwa jumla

Dhana muhimu katika sura hii

Milele

Sura hii inatofautisha vitu vya dunia hii ambavyo havidumu na kuishi kwa ajili ya vitu vitakavyodumu milele. Ni vyema pia kuishi na matarajio kwamba Yesu atarudi karibuni. (Tazama: rc://*/tw/dict/bible/kt/eternity)

Viapo

Wasomi wanatofautiana iwapo fungu hili linafundisha kwamba viapo vyote ni vibaya. Wasomi wengi wanakubaliana kwamba viapo vingine vinakubalika na badala yake Yakobo anawafundisha Wakristo kuwa na maadili.

Maswala mengine ya utata katika tafsiri ya sura hii

Eliya

Hadithi hii itakuwa ngumu kuelewa iwapo vitabu vya 1 Wafalme na 2 Wafalme na 1 Mambo ya Nyakati na 2 Mambo ya Nyakati havijatafsiriwa.

"Okoa roho yake kutoka kwa kifo"

Huenda hii inafundisha kwamba mtu anayeacha maisha yake ya dhambi hataadhibiwa na kifo cha mwili kama athari ya dhambi yake. Kwa upande mwingine, wasomi wamoja wanaamini kwamba hili fungu linafundisha kuhusu wokovu wa milele. (Tazama: [[rc:///tw/dict/bible/kt/sin]] and [[rc:///tw/dict/bible/other/death]] and rc://*/tw/dict/bible/kt/save)

__<< | __