sw_tn/jas/03/07.md

24 lines
964 B
Markdown

# Kila aina ya .... na mwanadamu.
Usemi huu "kila aina" humaanisha "aina nyingi." hii inaweza kutafsriwa kama fungu la maneno yanayoonesha kutenda; "Watu wamejifunza kudhibiti aina nyingi za wanyama wa mwitu, ndege, vitambaavyo, na viumbe wa baharini."
# Kitambaacho.
Huyu ni mnyama ambaye hutembea juu ya ardhi kwa kujikokota.
# Kiumbe wa baharini
Huyu ni mnyama ambaye anaishi majini.
# Lakini kuhusu ulimi hakuna hata mmoja miongoni mwa watu awezaye kuchunga ulimi.
Hapa "ulimi" humaanisha kile ambacho mtu hutamka. Maana kamili inaweza kutajwa kwa uwazi kama hivi: "hakuna mtu hata mmoja awezaye kudhibiti ulimi wake pasipo msaada wa Mungu."
# Muovu asiyedhibitiwa
Ulimi umezungumziwa kama vile ni uovu usioweza kudhibitiwa. Yakobo anafananisha na tamaa za mtu kuongea mambo maovu.
# Umejaa sumu ya kufisha
Yakobo anafananisha uwezo wa mtu kuongea mabaya kama vile nyoka au mmea wenye sumu. Sumu ni maneno yaumizayo ambayo yanaweza kusemwa kwa mtu.