# Kila aina ya .... na mwanadamu. Usemi huu "kila aina" humaanisha "aina nyingi." hii inaweza kutafsriwa kama fungu la maneno yanayoonesha kutenda; "Watu wamejifunza kudhibiti aina nyingi za wanyama wa mwitu, ndege, vitambaavyo, na viumbe wa baharini." # Kitambaacho. Huyu ni mnyama ambaye hutembea juu ya ardhi kwa kujikokota. # Kiumbe wa baharini Huyu ni mnyama ambaye anaishi majini. # Lakini kuhusu ulimi hakuna hata mmoja miongoni mwa watu awezaye kuchunga ulimi. Hapa "ulimi" humaanisha kile ambacho mtu hutamka. Maana kamili inaweza kutajwa kwa uwazi kama hivi: "hakuna mtu hata mmoja awezaye kudhibiti ulimi wake pasipo msaada wa Mungu." # Muovu asiyedhibitiwa Ulimi umezungumziwa kama vile ni uovu usioweza kudhibitiwa. Yakobo anafananisha na tamaa za mtu kuongea mambo maovu. # Umejaa sumu ya kufisha Yakobo anafananisha uwezo wa mtu kuongea mabaya kama vile nyoka au mmea wenye sumu. Sumu ni maneno yaumizayo ambayo yanaweza kusemwa kwa mtu.