sw_tn/isa/66/12.md

20 lines
748 B
Markdown

# Maelezo ya Jumla
Yahwe anaendelea kuzungumza juu ya Yerusalemu kana kwamba ilikuwa mama.
# kama mto ... kama kijito kinachomwagikia
Hii ina maana Mungu atasababisha watu wa mataifa kuleta kiasi kikubwa cha utajiri, ambacho kitakuwa cha kudumu kama mto na wingi.
# Utanyonya kando yake, kubebwa mikononi mwake, na kuchezeshwa juu ya magoti yake
Hii ina maana Yerusalemu itakuwa sehemu ya usalama na faraja kwa watu wa Mungu.
# kubebwa mikononi mwake, na kuchezeshwa juu ya magoti yake
Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "atakubeba mikononi mwake na kukurusha juu ya magoti yake kwa furaha"
# kwa hiyo nitakufariji, na utafarijiwa Yerusalemu
Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "kwa hiyo nitakufariji katika Yerusalemu"