# Maelezo ya Jumla Yahwe anaendelea kuzungumza juu ya Yerusalemu kana kwamba ilikuwa mama. # kama mto ... kama kijito kinachomwagikia Hii ina maana Mungu atasababisha watu wa mataifa kuleta kiasi kikubwa cha utajiri, ambacho kitakuwa cha kudumu kama mto na wingi. # Utanyonya kando yake, kubebwa mikononi mwake, na kuchezeshwa juu ya magoti yake Hii ina maana Yerusalemu itakuwa sehemu ya usalama na faraja kwa watu wa Mungu. # kubebwa mikononi mwake, na kuchezeshwa juu ya magoti yake Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "atakubeba mikononi mwake na kukurusha juu ya magoti yake kwa furaha" # kwa hiyo nitakufariji, na utafarijiwa Yerusalemu Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "kwa hiyo nitakufariji katika Yerusalemu"