sw_tn/isa/41/05.md

32 lines
932 B
Markdown

# Taarifa ya Jumla
Yahwe anaendelea kuzungumza.
# Visiwa hivi ... mwisho wa dunia
Misemo hii inawakilisha watu ambao wanaishi maeneo hayo. "Watu ambao huishi katika vsiwa ... watu ambao huishi katika mwisho wa dunia"
# Visiwa
Hii ina maana ya watu ambao huishi katika visiwa na katika nchi zinazopatikana au ng'ambo ya pili ya Bahari ya Mediteranea.
# mwisho wa dunia
Sehemu katika dunia ambazo zipo mbali sana na zinazungumziwa kana kwamba ni sehemu ambapo dunia huwa mwisho. "sehemu za mbali za dunia"
# vinakaribia na kuja
Hizi mbili zina maana ya kwamba watu hujikusanya pamoja. "wanakuja pamoja"
# fuawe
kipande cha chuma ambacho mtu kuchonga chuma kwa nyundo
# kusema juu ya kuchomelea
Hapa neno "kuchomelea" lina maana ya njia ya kukaza dhahabu kwa mbao pale ambapo watumishi humaliza kutengeneza sanamu.
# Wanaikaza kwa misumari ili kwamba isianguke
Hapa "isianguke" ina maana ya sanamu ambayo walitengeneza.