sw_tn/isa/14/18.md

1.4 KiB

Kauli Kiunganishi

Huu ni mwisho wa wimbo wa dhihaka ambao Waisraeli wataimba kwa mfalme wa Babeli.

wote watalala chini kwa heshima

Hii ina maana ya kwamba miili yao itazikwa kwa naman ya heshima. "wafalme wote ambao wamekufa wanazikwa kwa namna ya heshima"

Lakini umerushwa nje ya kaburi lako

Kurushwa nje ya kaburi inawakilisha kutozikwa. "lakini haujazikwa. Mwili wako umeachwa juu ya ardhi"

kama tawi lililotupwa

Tawi lilitupwa linawakilisha kitu kisichokuwa na thamani. "kama tawi lisilo na thamani ambalo hutupwa kando"

wafu wamekufunika kama vazi

Hii inawakilisha maiti nyingi kuwa juu ya mwili wake. "Miili ya wafu inafunika kabisa mwili wako" au "Miili ya wanajeshi waliokufa imerundikwa juu ya mwili wako"

wale waliochomwa kwa upanga

Hii inaelezea "wafu" ni kina nani katika mwanzo wa sentensi. Kuchomwa na upanga inawakilisha kuuliwa vitani. "wale ambao waliuliwa vitani"

wanaoshuka chini katika mawe ya shimo

Shimo lina maana aidha ya jehanamu, au shimo kubwa katika ardhi ambapo miili mingi ya wafu inatupwa.

Hautajiunga nao katika kuzikwa

Neno "nao" lina maana ya wafalme wengine ambao walikufa na kuzikwa vizuri. Kuwaunga katika kuzikwa inawakilisha kuzikwa kama wao. "hautazikwa kama wafalme wengine walivyozikwa"

Watoto wa waovu hawatatajwa tena

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "hakuna mtu atayezungumza tena kuhusu uzao wa waovu"