sw_tn/isa/14/18.md

36 lines
1.4 KiB
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2019-05-21 20:17:16 +00:00
# Kauli Kiunganishi
Huu ni mwisho wa wimbo wa dhihaka ambao Waisraeli wataimba kwa mfalme wa Babeli.
# wote watalala chini kwa heshima
Hii ina maana ya kwamba miili yao itazikwa kwa naman ya heshima. "wafalme wote ambao wamekufa wanazikwa kwa namna ya heshima"
# Lakini umerushwa nje ya kaburi lako
Kurushwa nje ya kaburi inawakilisha kutozikwa. "lakini haujazikwa. Mwili wako umeachwa juu ya ardhi"
# kama tawi lililotupwa
Tawi lilitupwa linawakilisha kitu kisichokuwa na thamani. "kama tawi lisilo na thamani ambalo hutupwa kando"
# wafu wamekufunika kama vazi
Hii inawakilisha maiti nyingi kuwa juu ya mwili wake. "Miili ya wafu inafunika kabisa mwili wako" au "Miili ya wanajeshi waliokufa imerundikwa juu ya mwili wako"
# wale waliochomwa kwa upanga
Hii inaelezea "wafu" ni kina nani katika mwanzo wa sentensi. Kuchomwa na upanga inawakilisha kuuliwa vitani. "wale ambao waliuliwa vitani"
# wanaoshuka chini katika mawe ya shimo
Shimo lina maana aidha ya jehanamu, au shimo kubwa katika ardhi ambapo miili mingi ya wafu inatupwa.
# Hautajiunga nao katika kuzikwa
Neno "nao" lina maana ya wafalme wengine ambao walikufa na kuzikwa vizuri. Kuwaunga katika kuzikwa inawakilisha kuzikwa kama wao. "hautazikwa kama wafalme wengine walivyozikwa"
# Watoto wa waovu hawatatajwa tena
Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "hakuna mtu atayezungumza tena kuhusu uzao wa waovu"