# Kauli Kiunganishi Huu ni mwisho wa wimbo wa dhihaka ambao Waisraeli wataimba kwa mfalme wa Babeli. # wote watalala chini kwa heshima Hii ina maana ya kwamba miili yao itazikwa kwa naman ya heshima. "wafalme wote ambao wamekufa wanazikwa kwa namna ya heshima" # Lakini umerushwa nje ya kaburi lako Kurushwa nje ya kaburi inawakilisha kutozikwa. "lakini haujazikwa. Mwili wako umeachwa juu ya ardhi" # kama tawi lililotupwa Tawi lilitupwa linawakilisha kitu kisichokuwa na thamani. "kama tawi lisilo na thamani ambalo hutupwa kando" # wafu wamekufunika kama vazi Hii inawakilisha maiti nyingi kuwa juu ya mwili wake. "Miili ya wafu inafunika kabisa mwili wako" au "Miili ya wanajeshi waliokufa imerundikwa juu ya mwili wako" # wale waliochomwa kwa upanga Hii inaelezea "wafu" ni kina nani katika mwanzo wa sentensi. Kuchomwa na upanga inawakilisha kuuliwa vitani. "wale ambao waliuliwa vitani" # wanaoshuka chini katika mawe ya shimo Shimo lina maana aidha ya jehanamu, au shimo kubwa katika ardhi ambapo miili mingi ya wafu inatupwa. # Hautajiunga nao katika kuzikwa Neno "nao" lina maana ya wafalme wengine ambao walikufa na kuzikwa vizuri. Kuwaunga katika kuzikwa inawakilisha kuzikwa kama wao. "hautazikwa kama wafalme wengine walivyozikwa" # Watoto wa waovu hawatatajwa tena Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "hakuna mtu atayezungumza tena kuhusu uzao wa waovu"