sw_tn/isa/06/08.md

28 lines
1.1 KiB
Markdown

# Taarifa ya Jumla
Isaya anaendelea kufafanua ono lake.
# sauti ya Bwana inasema
Hapa "sauti" inawakilisha Bwana mwenyewe. "Bwana anasema"
# nimtume nani
Inadokezwa ya kwamba Yahwe atamtuma mtu kuzungumza ujumbe wake kwa watu wa Israeli. "Nani nitamtuma kuwa mjumbe kwa watu wangu"
# nani ataenda kwa ajili yetu
Inaonekana "yetu" ina maana ya Yahwe na washiriki wa baraza lake la mbinguni.
# watu hawa
"watu wa Israeli"
# Sikilizeni, lakini msielewe; tazameni, lakini msitambue
Maana zawezekana kuwa 1) vitenzi vya kuamuru "msielewe" na "mstambue" vinaeleza kile Mungu anasababisha kufanyika. "Utasikia, lakini Yahwe hatakuruhusu uelewe; utatazama kwa makini, lakini Yahwe hataruhusu uelewe" au 2) vitenzi vya kuamuru "Sikiliza" na "tazama" zinaeleza wazo la "kama". "Hata kama ukisikiliza hautaelewa; hata kama utatazama kwa makini, hautaelewa"
# Sikilizeni, lakini msielewe; tazameni, lakini msitambue
Unaweza kueleza taarifa inayoeleweka kwa uwazi. "Sikiliza ujumbe wa Yahwe, lakini usielewe maana yake; tazama kile Yahwe anachofanya, lakini usigundue maana yake"