# Taarifa ya Jumla Isaya anaendelea kufafanua ono lake. # sauti ya Bwana inasema Hapa "sauti" inawakilisha Bwana mwenyewe. "Bwana anasema" # nimtume nani Inadokezwa ya kwamba Yahwe atamtuma mtu kuzungumza ujumbe wake kwa watu wa Israeli. "Nani nitamtuma kuwa mjumbe kwa watu wangu" # nani ataenda kwa ajili yetu Inaonekana "yetu" ina maana ya Yahwe na washiriki wa baraza lake la mbinguni. # watu hawa "watu wa Israeli" # Sikilizeni, lakini msielewe; tazameni, lakini msitambue Maana zawezekana kuwa 1) vitenzi vya kuamuru "msielewe" na "mstambue" vinaeleza kile Mungu anasababisha kufanyika. "Utasikia, lakini Yahwe hatakuruhusu uelewe; utatazama kwa makini, lakini Yahwe hataruhusu uelewe" au 2) vitenzi vya kuamuru "Sikiliza" na "tazama" zinaeleza wazo la "kama". "Hata kama ukisikiliza hautaelewa; hata kama utatazama kwa makini, hautaelewa" # Sikilizeni, lakini msielewe; tazameni, lakini msitambue Unaweza kueleza taarifa inayoeleweka kwa uwazi. "Sikiliza ujumbe wa Yahwe, lakini usielewe maana yake; tazama kile Yahwe anachofanya, lakini usigundue maana yake"