sw_tn/hos/12/01.md

28 lines
810 B
Markdown

# Taarifa ya jumla:
Nabii Hosea anazungumza.
# Efraimu hujilisha upepo
Wana wa Israeli wanafanya mambo ambayo hayatawasaidia ni sawasawa na kujilisha upepo.
# kufuata upepo wa mashariki.
Upepo wa mashariki ulikuwa na joto sana na wenye kuharibu. Hii inamaanisha kuwa majeshi kutoka mashariki ambayo Bwana atayatuma kuwaharibu wana wa Israeli.
# huchukua mafuta ya Misri
Wana wa Israeli walipeleka mafuta kama zawadi kwa mfalme wa Israeli na kumsihi awasaidie.
# Bwana pia ana mashtaka dhidi ya Yuda
Bwana anasema kwamba watu wa Yuda wamemtenda dhambi na kuvunja agano lake.
# dhidi ya Yuda ... ataadhibu Yakobo ... kwa yale aliyoyatenda ... atamlipa kwa matendo yake
"Yuda" na "Yakobo" wote wanawakilisha watu wa Yuda.
# mashitaka
Haya ni malalamiko ya mtu mmoja dhidi ya mtu mwingine mahakamani.