sw_tn/hos/09/05.md

32 lines
1001 B
Markdown

# Taarifa ya jumla
Nabii Hosea anazungumza.
# Utafanya nini siku ya sikukuu iliyowekwa rasmi, siku ya sikukuu ya Yahweh?
Hosea anatumia swali hili kusisitiza kuwa watu hawataweza kushuhudia sikukuu zao ikiwa adui watawashinda na kuwashukua mateka.
# siku ya sikukuu iliyowekwa rasmi ... siku ya sikukuu ya Yahweh
Zote hizi zina maana moja.
# Kama wamekimbia
Hapa wanazungumziwa wana wa Israeli.
# Misri itawakusanya, na Nofu itawazika
Misri na Nofu inamaanisha watu wanaoishi pale. "Jeshi la Wamisri litawakamata, mtakufa huko na watu wa mji wa Nofu watawazika"
# Maana hazina zao za pesa- michongoma mikali itakuwa nao
Michongoma imeota sehemu ambayo Israeli walihifadhi fedha zao michongoma hii imefananishwa na adui ambaye atakuja kuchukua mali wanazomiliki Waisraeli.
# michongoma itakuwa nao, na miiba itajaza hema zao.
"michongoma" na "miiba" inamaana moja. Michongoma na miiba ikiota inamanisha ardhi hiyo ni kama jangwa.
# Hema zao
Hapa "hema" inawakilisha nyumba za Waisraeli.