# Taarifa ya jumla Nabii Hosea anazungumza. # Utafanya nini siku ya sikukuu iliyowekwa rasmi, siku ya sikukuu ya Yahweh? Hosea anatumia swali hili kusisitiza kuwa watu hawataweza kushuhudia sikukuu zao ikiwa adui watawashinda na kuwashukua mateka. # siku ya sikukuu iliyowekwa rasmi ... siku ya sikukuu ya Yahweh Zote hizi zina maana moja. # Kama wamekimbia Hapa wanazungumziwa wana wa Israeli. # Misri itawakusanya, na Nofu itawazika Misri na Nofu inamaanisha watu wanaoishi pale. "Jeshi la Wamisri litawakamata, mtakufa huko na watu wa mji wa Nofu watawazika" # Maana hazina zao za pesa- michongoma mikali itakuwa nao Michongoma imeota sehemu ambayo Israeli walihifadhi fedha zao michongoma hii imefananishwa na adui ambaye atakuja kuchukua mali wanazomiliki Waisraeli. # michongoma itakuwa nao, na miiba itajaza hema zao. "michongoma" na "miiba" inamaana moja. Michongoma na miiba ikiota inamanisha ardhi hiyo ni kama jangwa. # Hema zao Hapa "hema" inawakilisha nyumba za Waisraeli.