sw_tn/heb/09/intro.md

1.6 KiB

Waebrania 09: Maelezo kwa jumla

Muundo na Mpangilio

Sura hii inaonyesha jinsi Yesu ni bora kuliko hekalu na sheria na masharti yake. Sura hii itakuwa ngumu kuelewa iwapo vitabo vitanu vya kwanza vya Agano la Kale havijatafsiriwa.

Dhana muhimu katika sura hii

Agano la urithi

Agano la urithi ni hati ya kisheria ambayo huelezea kile ambacho kitafanyikia mali ya mtu baada ya kifo chake.

Damu

Katika Agano la kale, Mungu alikuwa ameamuru Waisraeli kutoa dhabihu ili dhambi zao zisamehewe. Kabla hawajatoa dhabihu hizi, walipaswa kuwaua wanyama na siyo kutoa tu miili ya wanyama hao lakini pia damu zao. Kutoa damu ni tamathali ya kumuua binadamu ama mnyama.Mungu alipeana uhai na damu yake kama dhabihu/kafara alipowaruhusu watu kumuua.Mwandishi wa Waebrania anasema kwamba hii dhabihu ni bora kuliko dhabihu ya agano la kale.(Tazama: [[rc:///ta/man/translate/figs-metaphor]] and [[rc:///tw/dict/bible/kt/covenant]])

Kurudi kwa Kristo

Yesu atarudi kumaliza kazi aliyoianzisha wakati alipokufa ili Mungu angewasamehe watu dhambi zao. Atamalizia kuwaokoa watu wanaomngojea.(Tazama: rc://*/tw/dict/bible/kt/save)

Maswala mengine ya utata katika tafsiri ya sura hii

Agano la Kwanza

Hii inaashiria agano ambalo Mungu alifanya na Musa. Hata hivyo, kabla hajafanya agano hili, Mungu alikuwa amefanya agano na Abrahamu. Lakini hili lilikuwa ni agano la kwanza ambalo Mungu alifanya na watu wa Israeli. Unaweza amua kutafsiri "agano la kwanza" kama "agano la awali."

<< | >>