sw_tn/heb/06/04.md

36 lines
1.2 KiB
Markdown

# wale ambao waliipata nuru
uelewa unaongelewa kana kwamba ilikuwa ni kupatiwa nuru. AT: "wale ambao awali walielewa ujumbe kuhusu Kristo"
# ambao walionja kipawa cha mbinguni
kuonja wokovu kunaongelewa kana kwamba ni kuoonja chakula. AT: walionja nguvu ya Mungu ya kuokoa"
# kufanywa kuwa washirika wa Roho Mtakatifu,
Roho Mtakatifu ambaye anakuja kwa waumini, anaongelewa kana kwamba ni chombo ambacho watu wangeweza kushiriki. AT: "waliopoke Roho Mtakatifu"
# ambao walionja uzuri wa neno la Mungu
Kujifunza neno la Mungu kunaongelewa kana kwamba ilikuwa ni kuonja chakula. AT: "waliojifunza neno zuri la Mungu"
# nguvu za wakati ujao
Hii inamaanisha nguvuza Mungu wakati ufalme wake utakapo kuwa umetimilka duniani kote. kwa mantiki hii "nguvu" ina maanishaMungu mwenyewe, ambaye anamiliki nguvu zote.
# kisha wakaanguka
kupoteza uaminifu kwa Mungu kunaongelewa kana kwamba anguko la kimwili.AT: "walioacha kuamini katika Mungu"
# haiwezekani kuwarejesha tena katika toba
"Haiwezekani kuwarejesha tena kwenye toba"
# wamemsulubisha Mwana wa Mungu kwa nafsi zao
watu wanapoondoka kwa Mungu ni kana kwamba wanamsulubisha tena Yesu.
# Mwana wa Mungu
Hiki ni cheo muhimu ambacho kinaelezea uhusiano kwa Mungu.