sw_tn/heb/06/04.md

1.2 KiB

wale ambao waliipata nuru

uelewa unaongelewa kana kwamba ilikuwa ni kupatiwa nuru. AT: "wale ambao awali walielewa ujumbe kuhusu Kristo"

ambao walionja kipawa cha mbinguni

kuonja wokovu kunaongelewa kana kwamba ni kuoonja chakula. AT: walionja nguvu ya Mungu ya kuokoa"

kufanywa kuwa washirika wa Roho Mtakatifu,

Roho Mtakatifu ambaye anakuja kwa waumini, anaongelewa kana kwamba ni chombo ambacho watu wangeweza kushiriki. AT: "waliopoke Roho Mtakatifu"

ambao walionja uzuri wa neno la Mungu

Kujifunza neno la Mungu kunaongelewa kana kwamba ilikuwa ni kuonja chakula. AT: "waliojifunza neno zuri la Mungu"

nguvu za wakati ujao

Hii inamaanisha nguvuza Mungu wakati ufalme wake utakapo kuwa umetimilka duniani kote. kwa mantiki hii "nguvu" ina maanishaMungu mwenyewe, ambaye anamiliki nguvu zote.

kisha wakaanguka

kupoteza uaminifu kwa Mungu kunaongelewa kana kwamba anguko la kimwili.AT: "walioacha kuamini katika Mungu"

haiwezekani kuwarejesha tena katika toba

"Haiwezekani kuwarejesha tena kwenye toba"

wamemsulubisha Mwana wa Mungu kwa nafsi zao

watu wanapoondoka kwa Mungu ni kana kwamba wanamsulubisha tena Yesu.

Mwana wa Mungu

Hiki ni cheo muhimu ambacho kinaelezea uhusiano kwa Mungu.