sw_tn/heb/03/07.md

850 B

Sentensi Unganishi:

Onyo hapa ni ukumbusho kwamba kutokuamini kwa Waisraeli kuliwafanya wote kutoingia katika nchi ambayo Mungu alikuwa amewahidi. Kutokuamini kwao kulionyeshwa vizuri katika Kutoka 17:1, walipo mlalamikia Musa na kuwa na mashaka juu ya Mungu kama alikuwa pamoja nao.

Maelezo ya Jumla:

Nukuu hii inatoka katika Agano la Kale katika Zaburi.

kama mkisikia sauti yake

Amri za Mungu kwa Waisraeli zinaongelewa kana kwamba aliwakuwa amewapa katika sauti ya kusikika. AT: "kama mtasikia Mungu akiongea"

Msifanye mioyo yenu kuwa migumu

Ugumu wa moyo unaongelewa kana kwamba ni moyo halisi umefanywa kuwa mgumu. AT: "msiwewenye mioyo migumu"

kama katika uasi wakati wa kujaribiwa jangwani

Hapa "uasi" na "kujaribiwa" yanaweza kuelezewa kama vitenzi. AT: "kama vile na mababu zenu walivyo muasi Mungu na kumjaribu jangwani"