# Sentensi Unganishi: Onyo hapa ni ukumbusho kwamba kutokuamini kwa Waisraeli kuliwafanya wote kutoingia katika nchi ambayo Mungu alikuwa amewahidi. Kutokuamini kwao kulionyeshwa vizuri katika Kutoka 17:1, walipo mlalamikia Musa na kuwa na mashaka juu ya Mungu kama alikuwa pamoja nao. # Maelezo ya Jumla: Nukuu hii inatoka katika Agano la Kale katika Zaburi. # kama mkisikia sauti yake Amri za Mungu kwa Waisraeli zinaongelewa kana kwamba aliwakuwa amewapa katika sauti ya kusikika. AT: "kama mtasikia Mungu akiongea" # Msifanye mioyo yenu kuwa migumu Ugumu wa moyo unaongelewa kana kwamba ni moyo halisi umefanywa kuwa mgumu. AT: "msiwewenye mioyo migumu" # kama katika uasi wakati wa kujaribiwa jangwani Hapa "uasi" na "kujaribiwa" yanaweza kuelezewa kama vitenzi. AT: "kama vile na mababu zenu walivyo muasi Mungu na kumjaribu jangwani"