sw_tn/heb/01/intro.md

1.1 KiB

Waebrania 01 Maelezo kwa jumla

Muundo na Mpangilio

Sura hii inaonyesha jinsi Yesu ni muhimu kwa sisi kuliko malaika.

Watafsiri wengine wametenga kila mshororo wa ushairi kulia kuliko maandishi mengine ili isomeke kwa urahisi. ULB inafanya hivi na ushairi katika 1:5, 7-13, ambayo ni maneno kutoka Agano la Kale.

"Mababu wetu"

Mwandishi aliandikia barua hii Wakristo waliokuwa wamekua kama Wayahudi.Hii ndiyo maana barua hii inaitwa "Waebrania".

Mifano muhimu ya hotuba

Maswali ya hadithi

Mwandishi anatumia maswali ya hadithi kama njia ya kuthibitsha kwamba Yesu ni bora kuliko malaika. Yeye pamoja na wasomaji wake wanafahamu majibu ya maswali na mwandishi anajua kwamba wakati wasomaji wanafikiria juu ya majibu ya maswali, watakuja kufahamu kwamba Mwana wa Mungu ni muhimu kuliko malaika wowote.

Ushairi

Walimu Wayahudi sawa na manabii wa Agano la kale, waliyaweka masomo yao mengi ya muhimu kwa ushairi ili wasikilizaji waelewe na kuyakumbuka.

| >>