sw_tn/gen/41/42.md

24 lines
886 B
Markdown

# Farao akavua pete yake ya mhuri ... mkufu wa dhahabu shingoni mwake
Matendo haya yote yanaashiria ya kwamba Farao anampatia Yusufu mamlaka kufanya kila kitu ambacho Yusufu alipanga.
# pete ya mhuri
Pete hii ilikuwa na mhuri wa Mfalme uliochongwa juu yake. Hii ilimpatia Yusufu mamlaka na fedha iliyohitajika kutekeleza mipango yake.
# mavazi ya kitani safi
"Kitani" ni kitambaa kilaini, kigumu kinachotengenezwa na mmea wa kitani.
# Akataka apandishwe katika kibandawazi cha pili alichokuwa nacho
Tendo hili linadhihirisha wazi kwa watu ya kwamba Yusufu ni wa pili tu kutoka kwa Farao.
# Pigeni magoti
"Inama chini na mheshimu Yusufu". Kupiga goti na kuinama chini ilikuwa ishara ya heshima na taadhima.
# Farao akamweka juu ya nchi yote
Msemo "kukuweka juu" una maana ya kumpatia mamlaka. Hapa "nchi" ina maana ya watu. "Nimekupa mamlaka juu ya kila mmoja ndani ya Misri"