# Farao akavua pete yake ya mhuri ... mkufu wa dhahabu shingoni mwake Matendo haya yote yanaashiria ya kwamba Farao anampatia Yusufu mamlaka kufanya kila kitu ambacho Yusufu alipanga. # pete ya mhuri Pete hii ilikuwa na mhuri wa Mfalme uliochongwa juu yake. Hii ilimpatia Yusufu mamlaka na fedha iliyohitajika kutekeleza mipango yake. # mavazi ya kitani safi "Kitani" ni kitambaa kilaini, kigumu kinachotengenezwa na mmea wa kitani. # Akataka apandishwe katika kibandawazi cha pili alichokuwa nacho Tendo hili linadhihirisha wazi kwa watu ya kwamba Yusufu ni wa pili tu kutoka kwa Farao. # Pigeni magoti "Inama chini na mheshimu Yusufu". Kupiga goti na kuinama chini ilikuwa ishara ya heshima na taadhima. # Farao akamweka juu ya nchi yote Msemo "kukuweka juu" una maana ya kumpatia mamlaka. Hapa "nchi" ina maana ya watu. "Nimekupa mamlaka juu ya kila mmoja ndani ya Misri"