sw_tn/gen/41/33.md

28 lines
857 B
Markdown

# Maelezo ya Jumla:
Yusufu anaendelea kuongea na Farao.
# Basi
Hii haimaanishi "katika kipindi hiki" lakini inatumika kuvuta nadhari kwa lengo muhimu linalofuata.
# Farao atafute
Yusufu anazungumza na Farao katika lugha ya utatu. Hii ni namna ya kuonyesha heshima. Inaweza kuwekwa katika lugha ya upili. "Wewe, Farao, unapaswa kutafuta"
# kumweka juu ya nchi ya Misri
Msemo "kumweka juu" una maana ya kumpatia mtu mamlaka. "kumpatia mamlaka juu ya ufalme wa Misri" au "kumpa usimamizi juu ya ufalme wa Misri"
# nchi ya Misri
Hapa "nchi" ina maana ya watu wote na kila kitu ndani ya Misri.
# Na wachukue sehemu ya tano ya mazao ya Misri
Neno "tano" ni sehemu. "Na wagawanishe nafaka ya Misri katika sehemu tano za kufanana, kisha wachukue moja ya sehemu hizo"
# katika miaka saba ya shibe
"katika miaka saba ambayo kutakuwa na wingi wa chakula"