# Maelezo ya Jumla: Yusufu anaendelea kuongea na Farao. # Basi Hii haimaanishi "katika kipindi hiki" lakini inatumika kuvuta nadhari kwa lengo muhimu linalofuata. # Farao atafute Yusufu anazungumza na Farao katika lugha ya utatu. Hii ni namna ya kuonyesha heshima. Inaweza kuwekwa katika lugha ya upili. "Wewe, Farao, unapaswa kutafuta" # kumweka juu ya nchi ya Misri Msemo "kumweka juu" una maana ya kumpatia mtu mamlaka. "kumpatia mamlaka juu ya ufalme wa Misri" au "kumpa usimamizi juu ya ufalme wa Misri" # nchi ya Misri Hapa "nchi" ina maana ya watu wote na kila kitu ndani ya Misri. # Na wachukue sehemu ya tano ya mazao ya Misri Neno "tano" ni sehemu. "Na wagawanishe nafaka ya Misri katika sehemu tano za kufanana, kisha wachukue moja ya sehemu hizo" # katika miaka saba ya shibe "katika miaka saba ambayo kutakuwa na wingi wa chakula"