sw_tn/gen/37/34.md

28 lines
787 B
Markdown

# Yakobo akararua mavazi yake
Hili ni tendo la mawazo na uchungu mkubwa. Hii inaweza kuandikwa kwa uwazi zaidi. "Yakobo alikuwa na majonzi mpaka akararua nguo zake"
# kuvaa mavazi ya magunia katika viuno vyake
Hapa "viuno" ina maana ya sehemu ya katikati ya mwili au kiuno. "akavaa magunia"
# wakainuka
Hapa ujio wa watoto kwa baba yao inazungumziwa kama "kuinuka juu". "wakaja kwake"
# lakini alikataa kufarijiwa
Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "lakini hakutaka wamfariji"
# Hakika nitashuka kuzimu nikimwombolezea
Hii ina maana ataomboleza kutoka sasa hadi pale atakapokufa. "Kweli nitakapokufa na kwenda kuzimu bado nitakuwa naomboleza"
# Wamidiani wakamwuza
"Wamidiani walimuuza Yusufu"
# kepteni wa walinzi
"kiongozi wa wanajeshi waliokuwa wakimlinda mfalme"