# Yakobo akararua mavazi yake Hili ni tendo la mawazo na uchungu mkubwa. Hii inaweza kuandikwa kwa uwazi zaidi. "Yakobo alikuwa na majonzi mpaka akararua nguo zake" # kuvaa mavazi ya magunia katika viuno vyake Hapa "viuno" ina maana ya sehemu ya katikati ya mwili au kiuno. "akavaa magunia" # wakainuka Hapa ujio wa watoto kwa baba yao inazungumziwa kama "kuinuka juu". "wakaja kwake" # lakini alikataa kufarijiwa Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "lakini hakutaka wamfariji" # Hakika nitashuka kuzimu nikimwombolezea Hii ina maana ataomboleza kutoka sasa hadi pale atakapokufa. "Kweli nitakapokufa na kwenda kuzimu bado nitakuwa naomboleza" # Wamidiani wakamwuza "Wamidiani walimuuza Yusufu" # kepteni wa walinzi "kiongozi wa wanajeshi waliokuwa wakimlinda mfalme"