sw_tn/gen/34/11.md

20 lines
773 B
Markdown

# Shekemu akamwambia baba yake
"Shekemu alimwambia baba yake Dina Yakobo"
# Na nione kibari machoni penu, na chochote mtakachoniambia nitatoa
Hapa "machoni" ina maana ya fikra na mawazo ya mtu. "Kama utanipa kibali, basi nitakupa chochote utakachokiomba"
# mahari
Katika baadhi ya tamaduni, ni kawaida kwa mwanamume kutoa fedha, mali, ng'ombe, na zawadi zingine kwa familia ya mwanamke katika kipindi cha ndoa.
# Wana wa Yakobo wakamjibu Shekemu na Hamori baba yake kwa hila
Nomino inayojitegemea ya "hila" inaweza kuwekwa kama kitenzi cha "kudanganya". "Lakini wana wa Yakobo walimdanganya Shekemu na Hamori walipowajibu"
# Shekemu alikuwa amemnajisi Dina
Hii ina maana ya kwamba Shekemu aliwavunjia heshima sana na kumuabisha Dina kwa kumlazimisha kulala naye.