# Shekemu akamwambia baba yake "Shekemu alimwambia baba yake Dina Yakobo" # Na nione kibari machoni penu, na chochote mtakachoniambia nitatoa Hapa "machoni" ina maana ya fikra na mawazo ya mtu. "Kama utanipa kibali, basi nitakupa chochote utakachokiomba" # mahari Katika baadhi ya tamaduni, ni kawaida kwa mwanamume kutoa fedha, mali, ng'ombe, na zawadi zingine kwa familia ya mwanamke katika kipindi cha ndoa. # Wana wa Yakobo wakamjibu Shekemu na Hamori baba yake kwa hila Nomino inayojitegemea ya "hila" inaweza kuwekwa kama kitenzi cha "kudanganya". "Lakini wana wa Yakobo walimdanganya Shekemu na Hamori walipowajibu" # Shekemu alikuwa amemnajisi Dina Hii ina maana ya kwamba Shekemu aliwavunjia heshima sana na kumuabisha Dina kwa kumlazimisha kulala naye.