sw_tn/gen/30/01.md

20 lines
632 B
Markdown

# Raheli alipoona kwamba hamzalii Yakobo watoto
"Wakati Raheli alipogundua ya kwamba hawezi kupata mimba"
# nitakufa
Raheli anatumia ukuzaji kuonyesha jinsi alivyohuzunika ya kuhusu kutopata watoto. "Nitajisikia sina maana yoyote kabisa"
# Nipe watoto
"Nisababishie kupata mimba"
# Hasira ya Yakobo ikawaka juu ya Raheli
Hasira ya Yakobo inazungumziwa kana kwamba ilikuwa moto. "Yakobo alimkasirikia sana Raheli"
# Mimi ni badala ya Mungu, aliyekuzuilia usipate watoto?
Hili ni swali la balagha ambalo Yakobo anatumia kumkaripia Raheli. Inaweza kutafsiriwa kama kauli. "Mimi si Mungu! Mimi siye ninayekuzuia kupata watoto"