sw_tn/gen/24/10.md

28 lines
757 B
Markdown

# na akaondoka. Akachukua pia
Sentensi inayoanza na "Akachukua pia" inatupa taarifa ya nyongeza kuhusu nini mtumishi alichukua katika safari. Alivikusanya kabla ya kuondoka.
# Akachukua pia aina zote za zawadi kutoka kwa bwana wake
Hii ina maana alichukua pia vitu vingi ambavyo bwana wake alitaka akawapatie familia ya mwanamke.
# Akaondoka na kwenda
"akajiandaa na kuondoka" au "aliondoka na kwenda"
# mji wa Nahori
Maana zaweza kuwa 1) "mji ambapo Nahori aliishi" au 2) "mji ulioitwa Nahori".
# Akawapigisha magoti ngamia
Ngamia ni wanyama warefu wenye miguu mirefu. Aliwafanya wainamishe miguu yao na kushusha miili yao ardhini. "Aliwafanya ngamia kulala chini"
# kisima cha maji
"kisima cha maji" au "kisima"
# kuchota maji
"kufuata maji"