sw_tn/gen/23/07.md

44 lines
1.2 KiB
Markdown

# kusujudu
Hii ina maana ya kuinama au kupiga goti chini kabisa kwa kuonyesha unyenyekevu wa heshima na taadhima kwa mtu.
# kwa watu wa nchi ile, kwa wana wa Hethi
"kwa wana wa Hethi waliokuwa wakiishi katika eneo lile"
# wana wa Hethi
Hapa "wana" ina maana ya wale amabo wametoka kwa Hethi. "uzao wa Hethi"
# wafu wangu
Kivumishi kidogo "wafu" kinaweza kuelezwa kama kivumishi au kitenzi. "mke wangu aliyekufa" au "mke wangu ambaye amekufa"
# Efroni .... Sohari
Haya ni majina ya wanamume.
# pango la Makpela, ambalo analimiliki, ambalo liko mwishoni mwa shamba lake
"pango lake ambalo lipo mwishoni mwa shamba lililoko Makpela"
# pango la Makpela
"pango lililoko Makpela". Makpela ilikuwa jina ya eneo au sehemu. Efroni alimiliki shamba katika Makpela na pango ambalo lilikuwa katika shamba.
# ambalo analimiliki
Hii inatueleza jambo kuhusu pango lile. Efroni alimiliki pango lile.
# ambalo liko mwishoni mwa shamba lake
Hii pia inatumabia jambo kuhusu pango lile. Pango lilikuwa mwishoni mwa shamba la Efroni.
# aniuzie waziwazi
"niuzie mbele yenu wote" au "niuzie mbele ya uwepo wenu"
# kama miliki
"kama kipande cha nchi ambacho nitamiliki na kutumia"