# kusujudu Hii ina maana ya kuinama au kupiga goti chini kabisa kwa kuonyesha unyenyekevu wa heshima na taadhima kwa mtu. # kwa watu wa nchi ile, kwa wana wa Hethi "kwa wana wa Hethi waliokuwa wakiishi katika eneo lile" # wana wa Hethi Hapa "wana" ina maana ya wale amabo wametoka kwa Hethi. "uzao wa Hethi" # wafu wangu Kivumishi kidogo "wafu" kinaweza kuelezwa kama kivumishi au kitenzi. "mke wangu aliyekufa" au "mke wangu ambaye amekufa" # Efroni .... Sohari Haya ni majina ya wanamume. # pango la Makpela, ambalo analimiliki, ambalo liko mwishoni mwa shamba lake "pango lake ambalo lipo mwishoni mwa shamba lililoko Makpela" # pango la Makpela "pango lililoko Makpela". Makpela ilikuwa jina ya eneo au sehemu. Efroni alimiliki shamba katika Makpela na pango ambalo lilikuwa katika shamba. # ambalo analimiliki Hii inatueleza jambo kuhusu pango lile. Efroni alimiliki pango lile. # ambalo liko mwishoni mwa shamba lake Hii pia inatumabia jambo kuhusu pango lile. Pango lilikuwa mwishoni mwa shamba la Efroni. # aniuzie waziwazi "niuzie mbele yenu wote" au "niuzie mbele ya uwepo wenu" # kama miliki "kama kipande cha nchi ambacho nitamiliki na kutumia"