sw_tn/gen/07/01.md

36 lines
902 B
Markdown

# Taarifa ya jumla:
Matukio ya sura hii yanatokea baadaya Nuhu kujenga safina, kukusanya chakula, na kukiweka ndani ya safina.
# Njoo ...katika safina ...utakuja nao
"Ingia ... ndani ya safina .. chukua". Tafsiri nyingi husema "Nenda .. ndani ya safina .. chukua"
# wewe
Neno hapa "wewe" linamaana ya Nuhu la lipo katika umoja.
# nyumba yako
"familia yako"
# mwenye haki mbele yangu
Hii inamaana ya kwamba Mungu alimwona Nuhu kuwa mwenye haki.
# katika kizazi hiki
Hii inamaana ya watu wote ambao walikuwa wakiishi katika muda huo. "Kati ya watu wote wanaoishi sasa"
# mnyama aliye safi
Huyu alikuwa ni myama ambaye Mungu aliruhusu watu wake wamle na kutoa sadaka.
# wanyama wasio safi
Hawa ni wanyama ambao Mungu hakuruhusu watu wale au kutoa sadaka.
# kuhifadhi kizazi chao
"ili kwamba waweze kuwa na kizazi kitakachoishi" au "ili kwamba, baada ya gharika, wanyama waendelee kuishi"