# Taarifa ya jumla: Matukio ya sura hii yanatokea baadaya Nuhu kujenga safina, kukusanya chakula, na kukiweka ndani ya safina. # Njoo ...katika safina ...utakuja nao "Ingia ... ndani ya safina .. chukua". Tafsiri nyingi husema "Nenda .. ndani ya safina .. chukua" # wewe Neno hapa "wewe" linamaana ya Nuhu la lipo katika umoja. # nyumba yako "familia yako" # mwenye haki mbele yangu Hii inamaana ya kwamba Mungu alimwona Nuhu kuwa mwenye haki. # katika kizazi hiki Hii inamaana ya watu wote ambao walikuwa wakiishi katika muda huo. "Kati ya watu wote wanaoishi sasa" # mnyama aliye safi Huyu alikuwa ni myama ambaye Mungu aliruhusu watu wake wamle na kutoa sadaka. # wanyama wasio safi Hawa ni wanyama ambao Mungu hakuruhusu watu wale au kutoa sadaka. # kuhifadhi kizazi chao "ili kwamba waweze kuwa na kizazi kitakachoishi" au "ili kwamba, baada ya gharika, wanyama waendelee kuishi"