sw_tn/gen/01/16.md

40 lines
964 B
Markdown

# Mungu akafanya mianga mikuu miwili
"Kwa njia hii Mungu akafanya mianga miwili mikuu" Sentensi hii inaelezea Mungu alichofanya alipozungumza.
# mianga miwili mikuu
"mianga miwili mikuu" au "mianga miwili ing'aaro". Mianga miwili mikuu ni jua na mwezi.
# kutawala mchana
"kuongoza mchana kama mtawala angozapo kundi la watu" au "kuweka alama katika siku"
# siku
Hii inamaanisha masaa ya mchana pekee
# mwanga mdogo
"mwanga mdogo" au "mwanga hafifu"
# katika anga
"katika mbingu" au "katika uwazi wa angani"
# kutenganisha mwanga na giza
"kutenganisha mwanga na giza" au "kutoa mwanga kwa kipindi kimoja na giza kwa kingine.
# Mungu akaona kuwa ni vyema
Hapa "ni" inamaanisha jua, mwezi na nyota.
# jioni na asubuhi
Hii inamaanisha siku nzima. Mwandishi anazungumzia siku nzima kana kwamba ni sehemu mbili. Kwa tamaduni za Kiyahudi, siku moja huanza baada ya jua kuzama.
# siku ya nne
Hii inamaanisha siku ya nne ambapo ulimwengu ulianza kuwepo.