# Mungu akafanya mianga mikuu miwili "Kwa njia hii Mungu akafanya mianga miwili mikuu" Sentensi hii inaelezea Mungu alichofanya alipozungumza. # mianga miwili mikuu "mianga miwili mikuu" au "mianga miwili ing'aaro". Mianga miwili mikuu ni jua na mwezi. # kutawala mchana "kuongoza mchana kama mtawala angozapo kundi la watu" au "kuweka alama katika siku" # siku Hii inamaanisha masaa ya mchana pekee # mwanga mdogo "mwanga mdogo" au "mwanga hafifu" # katika anga "katika mbingu" au "katika uwazi wa angani" # kutenganisha mwanga na giza "kutenganisha mwanga na giza" au "kutoa mwanga kwa kipindi kimoja na giza kwa kingine. # Mungu akaona kuwa ni vyema Hapa "ni" inamaanisha jua, mwezi na nyota. # jioni na asubuhi Hii inamaanisha siku nzima. Mwandishi anazungumzia siku nzima kana kwamba ni sehemu mbili. Kwa tamaduni za Kiyahudi, siku moja huanza baada ya jua kuzama. # siku ya nne Hii inamaanisha siku ya nne ambapo ulimwengu ulianza kuwepo.