sw_tn/gen/01/14.md

44 lines
1.5 KiB
Markdown

# Kuwe na mianga katika anga
Hii ni amri. Kwa kuamuru ya kwamba mianga iwepo, Mungu alifanya iwepo
# mianga katika anga
"vitu ving'aavyo katika anga" au"vitu vitoavyo mwanga katika anga". Hii inaamanisha jua, mwezi na nyota
# katika anga
"katika uwazi wa anga" au "katika uwazi mkubwa wa anga"
# kutenganisha mchana na usiku
"kutenganisha mchana na usiku." Hii inamaanisha "kutusaidia kutambua tofauti kati ya mchana na usiku." Jua inamaanisha ni mchana, na mwezi na nyota humaanisha ni usiku.
# na ziwe kama ishara
Hii ni amri. Kwa kuamuru ya kwamba ziwe kama ishara, Mungu alizifanya zitumike kama ishara. "Na zitumike kama ishara" au "na zioneshe"
# ishara
Hapa inamaanisha kitu kinachofunua au kinacholenga jambo
# majira
"Majira" inamaanisha nyakati zitakazotengwa kwa sikukuu na mambo mengine ambayo watu hufanya.
# kwa majira, kwa siku na miaka
Jua, mwezi, na nyota huonyesha muendelezo wa muda. Hii inatusaidia kutambua ni wakati gani tukio hutokea kila wiki, mwezi au mwaka.
# ziwe mianga katika anga ili kutoa mwanga juu ya nchi
Hii ni amri. Kwa kuamuru ziwe mianga juu ya nchi, Mungu alifanya zimulike juu ya nchi
# kutoa mwanga juu ya nchi
"kutoa mwanga juu ya nchi" au "kuangazia nchi". Nchi haitoi mwanga yenyewe bali hupata mwanga na kurudisha mwanga.
# ikawa hivyo
"ilitokea kama hivyo" au "Hivyo ndivyo ilivyotokea". Mungu alichoamuru kilitokea kama alivyotamka kitokee. Msemo huu hujitokeza katika sura nzima na una maana ile ile kila unapojitokeza.