# Kuwe na mianga katika anga Hii ni amri. Kwa kuamuru ya kwamba mianga iwepo, Mungu alifanya iwepo # mianga katika anga "vitu ving'aavyo katika anga" au"vitu vitoavyo mwanga katika anga". Hii inaamanisha jua, mwezi na nyota # katika anga "katika uwazi wa anga" au "katika uwazi mkubwa wa anga" # kutenganisha mchana na usiku "kutenganisha mchana na usiku." Hii inamaanisha "kutusaidia kutambua tofauti kati ya mchana na usiku." Jua inamaanisha ni mchana, na mwezi na nyota humaanisha ni usiku. # na ziwe kama ishara Hii ni amri. Kwa kuamuru ya kwamba ziwe kama ishara, Mungu alizifanya zitumike kama ishara. "Na zitumike kama ishara" au "na zioneshe" # ishara Hapa inamaanisha kitu kinachofunua au kinacholenga jambo # majira "Majira" inamaanisha nyakati zitakazotengwa kwa sikukuu na mambo mengine ambayo watu hufanya. # kwa majira, kwa siku na miaka Jua, mwezi, na nyota huonyesha muendelezo wa muda. Hii inatusaidia kutambua ni wakati gani tukio hutokea kila wiki, mwezi au mwaka. # ziwe mianga katika anga ili kutoa mwanga juu ya nchi Hii ni amri. Kwa kuamuru ziwe mianga juu ya nchi, Mungu alifanya zimulike juu ya nchi # kutoa mwanga juu ya nchi "kutoa mwanga juu ya nchi" au "kuangazia nchi". Nchi haitoi mwanga yenyewe bali hupata mwanga na kurudisha mwanga. # ikawa hivyo "ilitokea kama hivyo" au "Hivyo ndivyo ilivyotokea". Mungu alichoamuru kilitokea kama alivyotamka kitokee. Msemo huu hujitokeza katika sura nzima na una maana ile ile kila unapojitokeza.